PAMOJA na ugumu unaonekana katika msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa Tanzania Prisons kushika nafasi ya pili kutoka mwisho, nyota wa timu hiyo hawajakubali kushindwa kwani bado wanaendelea kupiga hesabu za vidole hadi kieleweke.

Tanzania Prisons imeshinda mechi tatu pekee kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya Mbeya City (2-1), KMC (1-0) na Namungo (3-2), huku ikiambulia sare tano kati ya hizo imetoka 0-0 kila mechi dhidi ya Azam, Pamba Jiji, JKT Tanzania, Mashujaa na KMC ikipata sare ya 1-1, ina alama 14 baada ya kucheza mechi 21, zikiwamo 13 ilizopoteza. Imefunga mabao 11 na kururuhusu 28.

PRI 01

Akizungumzia hali hiyo, mshambuliaji wa Tanzania Prisons, George Mpole anayemiliki mabao manne, amesema: “Bado hatujashuka, tuna nafasi kubwa ya kupambana kuhakikisha timu inasalia Ligi Kuu Bara, ingawa mbele yetu kuna mechi ngumu dhidi ya Simba, hatutaacha kupambana hadi tone la mwisho.”

Mshambuliaji mwingine wa timu hiyo, Jeremiah Juma anayemiliki mabao mawili hadi sasa, amesema:

PRI 02

“Kihesabu bado hatujashuka, ingawa tutatakiwa kuvuja jasho kweli kweli kutokana na ugumu wa mechi za mwishoni ambazo kila timu ina mipango yake, lakini bado tuna hesabu kali na tutafanikiwa.”

Kipa wa timu hiyo, Mussa Mbisa aliye na cleansheets tano amesema: “Tuna wakati mgumu mno, lakini hesabu bado zinaturuhusu kupambana na kuwa na nafasi nyingine ya kuendelea kusalia Ligi Kuu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *