Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Arif Suleman Premji, ameishauri Serikali kuendelea kuwekeza zaidi katika elimu na teknolojia ili kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kujitegemea badala ya kutegemea ajira pekee baada ya kuhitimu.
Akichangia mjadala wa bajeti bungeni, Premji amesema lengo la kuwapeleka watoto shule linapaswa kuwa kuwapa maarifa na ujuzi wa kutatua changamoto za jamii na kubadili changamoto hizo kuwa fursa za ajira kwao na kwa wengine.
Amesema dunia imepiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia, lakini bado shule nyingi hasa za vijijini zinakabiliwa na uhaba wa kompyuta, hali inayochelewesha maendeleo ya elimu ya kidijitali.
Premji amesisitiza kuwa wizara inahitaji fedha zaidi ili kuongeza kasi ya uwekezaji katika miundombinu ya teknolojia shuleni, akisema hatua hiyo itasaidia taifa kwenda sambamba na mabadiliko ya dunia na kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050.
(Feed generated with FetchRSS)