Tarehe ya uchaguzi wa urais nchini Burundi, uliyopangwa kufanyika Mei 3, 2027, imetangazwa Ijumaa, Mei 8, 2026, na Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi (CENI). Katika taarifa ya pamoja, vyama vya upinzani CNL, UPRONA, CODEBU, DCP, na FRODEBU vimetaka kufanyika kwa mazungumzo ya kitaifa kama sharti la uchaguzi wowote.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Vyama vilivyotia saini vinabaini  vina hofu kujirudi kwa hali ya uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2025, wakati vililaani makosa mengi na, vikisikitishwa na kuona hakuna mageuzi yaliyotekelezwa tangu wakati huo. Kwa hivyo ombi lao: kufunguliwa kwa mazungumzo ya kisiasa katika ngazi ya kitaifa, wakisema, ili “kujifunza kutokana na yaliyopita”.”

“Ikiwa uchaguzi utapangwa kama tulivyoona mwaka wa 2025, kushiriki katika chaguzi kama hizo itakuwa ni uwongo, anasema Olivier Nkurunziza, Katibu Mkuu wa chama cha Uprona. Hili litasababisha matatizo zaidi katika mshikamano wa kijamii, kwa sababu hata CENI, ambayo huandaa uchaguzi, haiko huru leo. Bado tunahitaji kujadili hili na kuhakikishiwa kwamba wakati huu, taasisi hiyo iko huru kweli.”

“Wanaweka masharti kwa kushiriki kwao” katika uchaguzi

Msimamo unaolaaniwa na Doriane Munezero, Katibu wa chama tawala cha CNDD-FDD, anayehusika na mawasiliano: “Ni aibu. Chama cha CNDD-FDD kimejitolea kikamilifu kwa mfumo wa kisiasa unaoruhusu na kukubali uwepo wa vyama vingi, lakini demokrasia iliyokomaa, kama tunavyoielewa nchini Burundi, haiwezi kufanya kazi chini ya tishio la mara kwa mara la kususia wakati wa kila mzunguko wa uchaguzi. Kwa hiyo kuna kitu hakiko sawa. Wanaweka masharti kwa kushiriki kwao katika uchaguzi. Kwa hivyo, ni masikitiko makubwa kwa demokrasia ya Burundi.”

Kwa sasa, serikali haijajibu ombi hili la mazungumzo. Hata hivyo, CNDD-FDD tayari ilimteua mgombea wake kwa uchaguzi wa urais tangu Aprili 2026: rais wa sasa, Évariste Ndayishimiye.

Mnamo mwaka 2025, Agathon Rwasa, mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani na rais wa zamani wa CNL, alikataliwa na CENI (Tume Huru ya Ktaifa ya Uchaguzi kugombea ubunge.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *