Mkuu wa mkoa wa njombe Anthony Mtaka ameziasa taasisi za kidini kuongeza juhudi katika kuelimisha jamii kuhusu afya ili kuwasaidia wapate uelewa wa kutatua matatizo ya kiroho na ya kimwili.
Wito wa mkuu wa mkoa Anthony Mtaka ameutoa wakati akizindua kambi ya matibabu bure chini ya idara ya ATAPE Kupitia kanisa la Waadventista wasabato Njombe, huku akisisitiza taasisi zingine ziige mfano huo kuisaidia jamii.
Huduma mbalimbali zinatolewa katika kambi hii ya AFYA BURE chini ya idara ya atape, zikiwemo huduma za macho na upimaji wa magonjwa mbalimbali unaokwenda sambamba na kupewa matibabu na dawa bure.
Baadhi ya wakazi wa Njombe wanasema huduma hizi zimekuwa ni msaada mkubwa kwao, kwani gharama za matibabu kwa sasa ni kubwa nchini.
Viongozi wa serikali na wa dini kwa pamoja wanasema ushirikiano huu utaendelea ili kuhakikisha wanaisaidia jamii kiimani lakini zaidi ni kuisaidia jamii ipate uelewa wa masuala ya Afya ili kulinda nguvu kazi ya kanisa na Taifa kwa ujumla.
Huduma hizi zinaendelea kutolewa kwa muda wa wiki moja bure sambamba na utolewaji wa dawa bila malipo.
#Startvhabari
#RFAOnline
@dkhan1410

(Feed generated with FetchRSS)