‎#HABARI: Serikali ya Awamu ya Sita imetangaza maboresho makubwa ya kisera yatakayowezesha sekta binafsi kushiriki katika uwekezaji na usambazaji wa huduma za maji kupitia mfumo wa ubia (PPP).

Hatua hiyo inalenga kujenga “Gridi ya Taifa ya Maji” itakayounganisha huduma kwa ufanisi zaidi nchini kote, huku ikitumia teknolojia za kisasa katika uzalishaji na usimamizi wa rasilimali hiyo muhimu kwa wananchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Maji, Kundi Mathew, amebainisha kuwa mahitaji ya maji yanaongezeka kwa kasi kutokana na ukuaji wa miji na shughuli za kiuchumi, jambo linalohitaji mitaji mikubwa kutoka sekta binafsi.

Kupitia ushirikiano huo, Serikali inakusudia kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi mijini na vijijini pamoja na kupunguza upotevu wa maji kwa kutumia mifumo ya kidigitali.

Maboresho haya yanatarajiwa kufungua fursa mpya za ajira, kuchochea ubunifu wa kiteknolojia, na kuimarisha ufanisi wa taasisi za maji nchini.

Aidha, ushiriki wa sekta binafsi utasaidia kuvutia utaalamu wa kisasa utakaohakikisha kila Mtanzania anapata huduma ya maji ya uhakika, jambo litakalochochea ustawi wa sekta za afya na viwanda.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *