Wadau wa sekta ya fedha kutoka nchi zaidi ya 40 wamekutana jijini Arusha kujadili namna ya kuboresha sera na mikakati ya kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa wananchi.

Mkutano huo umefunguliwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Sauda Msemo, ambaye amesema matumizi ya teknolojia za kifedha na sera imara vitasaidia kuondoa vikwazo vinavyowazuia wananchi kupata huduma za fedha.

Kwa upande wake, Eliki Boletawa wa Alliance for Financial Inclusion amesema ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana uzoefu vitasaidia kupata suluhisho bora la changamoto za sekta ya fedha.

✍ Ramadhani Mvungi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *