#HABARI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, ametoa agizo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha suala la usafi wa mazingira linakuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyote kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa.
Akifungua mkutano wa tathmini ya udhibiti wa taka ngumu jijini Dodoma, Prof. Shemdoe amesisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kufanya miji na majiji kuwa masafi, jambo litakalosaidia kupunguza milipuko ya magonjwa na kuokoa fedha za matibabu ili zielekezwe kwenye miradi mingine ya maendeleo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu (Afya), Prof. Tumaini Nagu, amebainisha kuwa udhibiti madhubuti wa taka ngumu una uwezo wa kupunguza magonjwa kama Malaria kwa asilimia 30 hadi 40.
Aidha, mkutano huo wenye kaulimbiu isemayo “Taka ngumu ni Mali; tumia, rejeleza na Weka Miji katika hali ya usafi”, umehimiza ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika ukusanyaji na uchakataji wa taka ili kuongeza ufanisi wa utunzaji wa mazingira nchini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)