Wizara ya Afya ya Lebanon imetangaza katika taarifa siku ya Jumanne kwamba watu 13 waliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel yaliyolenga maeneo matatu kusini mwa Lebanon.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

“Shambulio katika mji wa Nabatieh lilmewaua watu watano, wakiwemo wafanyakazi wawili wa ulinzi wa raia, na kuwajeruhi wengine wawili,” wizara iliripoti. Shambulio jingine katika mji wa Jebchit liliwaua watu wanne, akiwemo mwanajeshi mmoja na raia wa Syria, na kuwajeruhi wengine 12. Shambulio la tatu huko Bint Jbeil liliwaua raia wanne, akiwemo mtoto mmoja, na kuwajeruhi wengine wawili, kulingana na chanzo hicho.

Jeshi la Lebanon lilitangaza mapema katika taarifa kifo cha mwanajeshi aliyeuawa katika shambulio la anga la Israel huko Jebchit.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *