Baadhi ya wazee waliokuwa wanachama wa Chama cha Ushirika cha Mikahawa wamemuomba rais Dkt. Samia kuingilia kati na kuwarejeshea majengo yao ya biashara yaliyochukuliwa kimabavu na Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Gerezaji Jijini Dar es salaam.
Wazee hao ambao wamekutana na waandishi wa habari, wamesema kwa nguvu zao walijenga majengo kwa msaada wa wafadhili kabla ya CCM kuomba vyumba 32 kwaajli ya ofisi mwaka 1973, lakini baada ya hapo chama hicho kikajimilikisha eneo hilo zilipo ofisi za chama hicho Kata ya Gerezani Manispaa ya Ilala.
Akijibu shutuma hizo kwa njia ya simu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ali Bananga, amekiri kuwepo kwa mgogoro huo ambao hata hivyo chama hicho kilishinda kesi Mahakamani.
(Feed generated with FetchRSS)