Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepewa wiki moja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwasilisha maelezo kuhusu madai ya kukiuka masharti ya Sheria ya vyama vya siasa katika shughuli zake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Sisty Nyahoza kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa, chama hicho kimetakiwa kueleza sababu zinazoweza kuzuia usajili wake kusimamishwa au kutozwa faini kutokana na madai ya ukiukwaji wa sheria pamoja na masharti ya usajili.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa CHADEMA inapaswa kuwasilisha maelezo hayo kabla ya Mei 20 mwaka huu.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *