Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameivunja Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), miezi 14 baada ya kuzinduliwa.

Bodi hiyo ilizinduliwa Machi 27 mwaka jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumisii wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwan Kikwete.

Bodi hiyo ilikuwa inaongozwa na Joyce Mapunjo  akiwa mwenyekiti na wajumbe wangine wanane, ambao ni Tumaini Nyamhokya, Suzanne Doran na Fortunatus Magambo.

Wajumbe wengine wa bodi hiyo walikuwa Sadi Shemliwa, Vicky Jengo, Dk Haphsa Hincha, Pius Maneno na Emma Lyimo.

Taarifa ya kuvunjwa kwa bodi hiyo imetolewa Mei 14, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka kupitia taarifa ilitiwa saini na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Shaaban Kissu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *