Kihongosi aeleza CCM inavyopika viongoziKihongosi aeleza CCM inavyopika viongozi

Bunda. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema mbali na kuwa na jukumu la siasa nchini lakini chama hicho kimekuwa sehemu muhimu ya kuwaandaa viongozi bora ambao wamekuwa na mchango chanya katika maendeleo ya nchi na watu wake.

Kauli hiyo imetolewa mjini Bunda leo Jumapili, Mei 17, 2026 wakati akihutubia mkutano wa hadhara.

Amesema chama hicho kimekuwa kikifanya hivyo kutokana na ukweli kuwa masilahi ya nchi ni kipaumbele chake.

Amesema wapo viongozi wengi ambao wametokana na chama hicho na kushika nyadhifa mbalimbali katika sekta mbalimbali ikiwamo serikalini na kutimiza wajibu wao vizuri na hatimaye kuleta matokeo chanya katika maeneo yao ya uongozi.

“Wapo wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na viongozi wa nafasi mbalimbali ndani na nje ya nchi ambao ni mazao ya CCM na wamekuwa viongozi bora wenye kuleta tija katika nafasi zao kutokana na mafunzo mazuri ya uongozi na uzoefu waliopata kupitia CCM,” amesema.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Kenani Kihongosi, akihutubia mkutano wa hadhara mjini Bunda ikiwa ni sehemu ya mwisho ya zaira yake mkoani Mara

Kihongosi amesema uongozi sio mhemko wala kufarakanisha watu badala yake ni kutanguliza masilahi ya Taifa mbele, hivyo chama hicho kwa kuona umuhimu huo ndio maana kimekuwa na utaratibu wa kuwafunda viongozi kuanzia wakiwa na umri mdogo ili kuweza kuwatumikia Watanzania kwa nafasi mbalimbali.

Amesema hakuna chama kingine chenye utaratibu kama huo jambo ambalo pamoja na mambo mengine linasababisha vyama hivyo kutokuwa na sifa na uwezo wa kuongoza nchi.

“Tuna utaratibu wa kuwapika viongozi kulingana na umri wao kabla hatujawatuma kuwatumikia wananchi kupitia nafasi mbalimbali, tunaanza na chipukizi kisha vijana na jumuiya za chama kabla ya kwenda kwenye nafasi za juu,” amesema.

Kihongosi amesema kutokana na hali hiyo chama hicho ndicho  chama pekee chenye uwezo wa kuwangoza Watanzania na kuwaletea maendeleo kwani hakibahatishi na kwamba suala la uongozi bora ni sehemu ya ajenda zake.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Kenani Kihongosi, akihutubia mkutano wa hadhara mjini Bunda ikiwa ni sehemu ya mwisho ya zaira yake mkoani Mara

Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi amesema jukumu la watumishi wa Serikali katika mkoa huo ni kuhakikisha wanatekeleza kwa ukamilifu ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/30.

“Sisi watumishi wa Serikali mkoani Mara tunatambua uwepo wa  mkataba kati ya wananchi na CCM na jukumu letu ni kuhakikisha kuwa mkataba huo unatekelezwa kwa ukamilifu wake,” amesema.

Kanali Mtambi amesema jukumu la watumishi hao wa Serikali mkoani humo ni kuhakikisha fedha zote zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati na ile ya kutoa huduma inatekelezwa ili wananchi wawe na maisha bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *