Trump aionya Iran, aitaka iharakishe upatikanaji wa makubalianoTrump aionya Iran, aitaka iharakishe upatikanaji wa makubaliano

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa onyo jipya kwa nchi ya Iran, akisema inatakiwa iharakishe ili kupata mkataba wa amani au vinginevyo hakutakuwa na kitu kitakachosalia kwenye nchi hiyo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Onyo la Trump linakuja wakati huu Washington ikijaribu kila namna kuishawishi Iran kukubali mapendekezo yake ya mpango wa amani, mapendekezo ambayo Tehran inasema haiwezi kuyakubali sababu mengine haya msingi.

Kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, rais Trump amesema muda hauko tena na Iran na kwamba haraka sana wakubali mpango wa amani ulioko mezani ama vinginevyo ataiharibu nchi hiyo.

Onyo lake pia linakuja siku chache tangu ahitimishe ziara nchini China, ambako katika mazungumzo na mwenyeji wake Xi Jinping, walikubaliana kuhakikisha mlango bahari wa Hormuz unasalia wazi, suala ambalo hadi sasa ni miongoni mwa maeneo ambayo Iran na Washington wanatofautiana pakubwa.

Marekani inataka Iran kuachana kabisa na urutubishaji wa nyuklia pamoja na kufungua mlango bahari wa Hormuz, madai ambayo Tehran inasema hayakubaliki kwakuwa suala la Nyuklia ni kuingilia Uhuru wake na kufungua bahari yake wakati Washington imeweka kizuizini ni jambo lisilokubalika.

Hata hivyo onyo hili la Trump si la kwanza tangu alipotangaza kusitisha vita kwa muda na Iran, wadadisi wa mambo wakisema Washington inatafuta njia ya kujiondoa kwenye mzozo unaoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *