WHO inaendelea na tathmini yake kuhusu mlipuko wa virusi vya HantaWHO inaendelea na tathmini yake kuhusu mlipuko wa virusi vya Hanta

Shirika la Afya Duniani limesema linaendeleza tathmini yake ya mlipuko wa virusi vya Hanta kama “hatari ndogo”, wakati huu meli ya kitalii ambayo mlipuko huo ulianzia ikikaribia kutia nanga kwenye bandari ya Uholanzi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

WHO inasema imekuwa ikifuatilia mwenendo wa virusi hivyo na kwa mujibu wa taarifa zilizopo sasa, bado hatari yake kwa dunia  ni ya chini.

Hata hivyo WHO inasema huenda kukaripotiwa maambukizi mapya miongoni mwa abiria na mabaharia waliokuwa kwenye meli ya MV Hondius, wakati huu uwezo wa kusambaa umedhibitiwa kufuatia mikakati iliyowekwa wakati wa kuwaondoa abiria kwenye meli hiyo.

Meli hiyo inatarajiwa kutia nanga baadaye leo katika bandari ya Rotterdam Uholanzi , ikiwa na watu 27  ambao 25 ni wafanyakazi na wawili na wahudumu wa afya.

Watu watatu walithibitishwa kufariki kwenye mlipuko huo ,huku raia mmoja wa Ufaransa ,mwanamke mwenye umri wa miaka 25 akithibitishwa kuambukizwa na kulazwa katika hospital ya Paris akiwa mahututi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *