Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na BRAC Maendeleo Tanzania wamekubaliana kuimarisha usambzaji na matumizi ya taarifa za h…Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na BRAC Maendeleo Tanzania wamekubaliana kuimarisha usambzaji na matumizi ya taarifa za h…

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na BRAC Maendeleo Tanzania wamekubaliana kuimarisha usambzaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa nchini.

Kikao hicho kimeongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt Ladislaus Chang’a na kusema kuwa ni fursa kwa taasisi hizo kuelewana na kuchunguza maeneo ya ushirikiano katika huduma za hali ya hewa.

Ameongeza kuwa kikao hicho kitasaidia kuchukua tahadhari za mapema na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa TMA ipo katika mageuzi ya kidigitali yanayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwa njia za kisasa.

Dkt Chang’a ameeleza dhamira ya TMA kuendelea kuboresha huduma za hali ya hewa na ushawishi wa Tanzania katika masuala ya hali ya hewa katika Bara la Africa na ukanda wa nchi zinazoendelea.

Kwa upande wake, Degefu Getachew Kelbiso, Meneja Mwandamizi wa Programu ya Hali ya Hewa ya Kimataifa na BRAC Maendeleo Tanzania, ameeleza kuhusu mpango wa “BigBet” unaolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia huduma za taarifa za hali ya hewa, kilimo kinachozingatia mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi, masoko na uimarishaji wa maisha ya jamii katika nchi kadhaa ikiwamo Tanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *