Dunia inazidi kuwa dhaifu kutokana na milipuko ya magonjwa ya kuambukizaDunia inazidi kuwa dhaifu kutokana na milipuko ya magonjwa ya kuambukiza

Wataalamu wameonya kuwa dunia inazidi kuwa dhaifu kutokana na milipuko ya magonjwa ya kuambukiza, wakati huu mamlaka za afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda zikijitahidi kudhibiti mlipuko wa Ebola.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya wataalam hao kuhusu majanga inajiri wakati huu ambapo dunia inakabiliwa pia na maambukizo ya Virusi vya Hanta barani Ulaya.

Aidha wameonya kuwa milipuko ya magonjwa inaendelea kuongezeka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mizozo inayoripotiwa katika maeneo mbalimbali ya dunia, ambapo kulingana na wataalam hao, dunia inahitaji kuweka nguvu pamoja kudhibiti milipuko ya magonjwa.

Ripoti hii inajiri wakati ambapo Shirika la afya duniani WHO likiwa limewatuma maofisa wake nchini DRC kusaidia juhudi za kudhibiti mlipuko wa Ebola kusambaa zaidi.

Ijumaa ya wiki hii, wanasayansi wa WHO watakutana kujadili kuhusu ugonjwa wa Ebola na namna kuimarisha vipimo vya uchunguzi na kutegeneza chanjo ya aina hii hatari zaidi ya virusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *