Mikoa hii ijipange kwa upepo mkali kuanzia keshoMikoa hii ijipange kwa upepo mkali kuanzia kesho

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza matarajio ya uwepo wa upepo mkali wa kilomita 40 kwa saa katika mikoa mitano nchini.

Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara pamoja na Unguja na Pemba hali inayotarajiwa kuwa mbaya kwa siku tano.

Kulingana na taarifa hiyo iliyotolewa leo Jumanne, Mei 19, 2026 na TMA, kuanzia kesho Jumatano angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya kaskazini mwa bahari ya Hindi.

“Ukanda huo unajumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), uwezekano wa kutokea athari ni wastani,” taarifa hiyo imeeleza.

Athari zinazoweza kujitokeza ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini.

Kwa siku ya Alhamisi angalizo lililotolewa la upepo wa kilomita 40 kwa saa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya kaskazini mwa bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

Uwezekano wa kutokea athari kulingana na taarifa hiyo ya TMA ni wastani na athari zinazoweza kujitokeza ni kusimama kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini.

Ijumaa ya Mei 22, kutakuwa na upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa  kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya kaskazini mwa bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

“Uwezekano wa kutokea athari ni wastani, kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini,”taarifa hiyo imeeleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *