
Baada ya miaka kumi akiwa madarakani nchini Benin, rais Patrice Talon anajiandaa kukabidhi hatamu ya uongozi wa nchi siku ya Jumapili hii, Mei 24, 2026 kwa msindi wa uchaguzi, waziri wake wa zamani wa fedha, Romuald Wadagni, aliyeshinda uchaguzi wa urais mwezi Aprili 2026. Huko Cotonou, ni wakati wa kuaga na kutafakari.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Cotonou, Jean Luc Aplogan
Siku ya Jumatano, rais anayeondoka madarakani aliongoza mkutano wake wa mwisho wa Baraza la Mawaziri. Msemaji wa serikali Wilfried Houngbédji alifanya mkutano wa mwisho na waandishi wa habari wa kitaifa na kimataifa. Katika ajenda: kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi wa shirika la utangazaji la Benin (SRTB), mapitio ya muongo mmoja madarakani, na suala la wafungwa wa kisiasa.
Mada ya kwanza ilikuwa kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi 169 wa shirika la utangazaji la SRTB, hatua ambayo ilichukuliwa Mei 13, 2026. Wilfried Houngbédji alivitaka vyombo vya habari kuoliza uongozi wa shirika hilo ili kupata maelezo zaidi. Hata hivyo, msemaji wa serikali alielezea masikitiko yake kwamba wafanyakazi husika waliarifiwa hatua hiyo dakika za mwisho. “Kibinadamu, ni jambo la kusikitisha,” alisema.
Mambo yako sawa
Kuhusu rekodi ya rais Patrice Talon, ambaye atamkabidhi madaraka Romuald Wadagni Mei 24, Wilfried Houngbédji alizungumzi hali halisi ya mambo, akipitia mageuzi makubwa yaliyofanywa. Kuhusu mageuzi ya kisiasa, ambayo yanapingwa mara kwa mara na upinzani, msemaji huyo aliyatetea kwa uthabiti: “Hatuna miaka hamsini ya mazoezi endelevu ya kidemokrasia nchini Benin. Nchi za Magharibi hutumia demokrasia tofauti. Kanuni ni sawa. Lazima tuzipitishe na kuzibadilisha.” Haikuwa na maana kwetu kuiga wengine katika kile ambacho wamekuwa wakifanya kwa miaka 300, wakati mwingine miaka 500.
Msamaha wa rais?
Swali lingine: Je, msamaha wa rais bado unawezekana kwa Reckya Madougou, Joel Aivo, Olivier Boko, na wafungwa wengine kabla ya Jumapili? Kwa Wilfried Houngbédji, “Katika saa 96, mambo mengi yanaweza kutokea, ikiwa ni pamoja na mambo ambayo hamyatarajii, na labda hata mambo mnayotarajia yanaweza yasitokee.” Aliongeza: “Hawa ni wanasiasa walio gerezani kwa makosa mbalimbali; hilo haliwafanyi kuwa wafungwa wa kisiasa.”
