Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na Majanga, Dkt. Erasto Sylvanus, amesema serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha ugonjwa wa Ebola hauingii nchini.
Dkt. Sylvanus amesema pamoja na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa huo katika baadhi ya mataifa, serikali haijazuia shughuli za kibiashara na usafiri baina ya nchi hizo na Tanzania, bali imeongeza ufuatiliaji na tahadhari katika mipaka na maeneo ya kuingilia wasafiri.
Amefafanua kuwa wasafiri hufanyiwa uchunguzi kabla ya kuingia au kutoka nchini, huku hatua za haraka zikichukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika kuwa na dalili zinazohusiana na Ebola.
✍Halima Abdallah
Mhariri | John Mbalamwezi
@goodluckpaul_mc
@balqis_njuki
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)
