MKuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa ahadi ya Sh50 milioni kwa Timu ya Mpira wa Kikapu Dar City endapo itafunz…MKuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa ahadi ya Sh50 milioni kwa Timu ya Mpira wa Kikapu Dar City endapo itafunz…

MKuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa ahadi ya Sh50 milioni kwa Timu ya Mpira wa Kikapu Dar City endapo itafunzu mtanange wake shidi ya Rwanda na kufikia hatua ya nusu fainali.

RC Chalamila ameyasema hayo katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JK Nyerere Terminal III wakati akiiaga timu hiyo kuelekea Kigali Rwanda kwenye mashindano.

Aidha, RC Chalamila ametoa amewataka wakazi wa mkoa huo endapo watabaini kuna kijana anakipaji cha basket ball,wamlete ofisini kwake ili aweze kuendelezwa kipaji hicho pamoja na kumuunganisha na wachezaji nguli wa Dar City Basket Ball.

Vilevile RC Chalamila amesema Rais wa timu hiyo, Hashimu Thabit akirudi toka Rwanda uandaliwe utaratibu wa kukutana na wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote wa mkoa kuona namna ya kuwa na uwanja mkubwa wa kisasa wa Basket Ball katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema Dar City ni timu ya kimataifa na inafanya vizuri ni ya kihistoria toka Tanzania ipate uhuru hivyo anaitakia kila kheri.

RC Chalamila amemshukuru Rais Samia kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya michezo kwa kuwa michezo ni afya lakini pia michezo ni uchumi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *