Nyota watano wanaotarajiwa kung’ara wakati wa michuano ya kombe la Dunia.Nyota watano wanaotarajiwa kung’ara wakati wa michuano ya kombe la Dunia.

Wasiwasi kuhusu kiwango cha uchezaji na utimamu wa mwili umeanza kuenea kwa baadhi ya mastaa wakubwa wa soka, huku zikiwa zimesalia wiki tatu tu kabla ya Kombe la Dunia kuanza, RFI Kiswahili tunawamulika wachezaji hao.

Imechapishwa:

Dakika 5 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na Hannah Nalianya

Kylian Mbappe (Ufaransa)

Mashambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappé.
Mashambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappé. © AP – Jose Breton

Mbappe anaweza kuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya Kombe la Dunia ndani ya wiki chache zijazo, lakini atafikia hili akiwa ametoka katika kipindi kigumu kule Real Madrid.

Mchezaji huyo mwenye miaka 27 bado hajashinda taji kubwa lolote katika misimu miwili akiwa na mabingwa hao wa Hispania licha ya rekodi yake bora ya ufungaji.

Kujitolea kwake kulihojiwa baada ya kwenda likizo huku akiuguza jeraha la misuli ya nyuma ya paja mwishoni mwa msimu.

Kubadilisha mazingira kupitia timu ya taifa huenda kukawa kile anachohitaji ili kuendelea kuandika historia kwenye jukwaa la dunia.

Mbappe aliitikisa dunia akiwa kijana wakati Ufaransa ilipotwaa Kombe la Dunia mwaka 2018.

Pia alifunga mabao nane, ikiwemo hat-trick katika fainali, wakati Les Bleus walipoteza kwa penalti dhidi ya Argentina miaka minne iliyopita.

Anahitaji mabao manne pekee kusawazisha rekodi ya Miroslav Klose ya mabao 16 katika fainali za Kombe la Dunia.

Erling Haaland (Norway)

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City ya Uingereza na timu ya taifa ya Norway, Erling Haaland.
Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City ya Uingereza na timu ya taifa ya Norway, Erling Haaland. © Dave Thompson/AP

Haaland hatimaye ataonja ladha ya mashindano makubwa ya kimataifa kwa mara ya kwanza baada ya Norway kumaliza ukame wa miaka 28 ya kufuzu Kombe la Dunia.

Mshambuliaji huyo wa Manchester City alifunga mara 16 katika michezo minane wakati wa kampeni bora ya kufuzu ya Norway iliyojumuisha ushindi mkubwa mara mbili dhidi ya Italia.

Ushindi huo ulimafanya kufikisha mabao 55 katika mechi 49 za kimataifa.

Haaland ni sura kuu ya kizazi kipya cha wachezaji wa Norway, akiwemo nahodha wa Arsenal, Marti Odegaard, ambao wamejumuishwa katika kikosi.

Hata hivyo, Norway itamhitaji mshambuliaji huyu kuwa katika kiwango bora baada ya kupangwa kundi gumu kando ya Ufaransa na mabingwa wa Afrika Senegal.

Vinicius Junior (Brazil)

Vinícius Júnior, winga mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil.
Vinícius Júnior, winga mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil. © AP Photo/Jose Breton

Kurejea kwa Neymar katika kikosi cha Brazil kumewavutia wengi, lakini kiwango cha Vinicius ndicho kitakachoamua kama kikosi cha Carlo Ancelotti kitaongeza nyota ya sita kwenye jezi maarufu ya njano.

Yeye na Mbappe wamekuwa wakigawana umaarufu mjini Madrid, lakini Kombe la Dunia linampa Vinicius nafasi ya kuwa shujaa wa taifa nchini Brazil na kushinda tuzo ya Ballon d’Or anayotamani.

Vinicius na wachezaji wenzake wa klabu ya Real Madrid waligomea hafla ya utoaji wa tuzo baada ya kupuuzwa na kiungo Rodri wa Manchester City kushinda tuzo hiyo.

Lakini rekodi yake akiwa na Brazil si ya kuridhisha kwani amefunga bao moja pekee katika Kombe la Dunia lililopita na ana mabao manane tu katika mechi 47 za kimataifa.

Harry Kane (Uingereza)

Harry Kane, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Bayern Munich.
Harry Kane, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Bayern Munich. AFP – OSCAR DEL POZO

Nahodha na mfungaji bora wa muda wote wa Uingereza anaingia katika kile kinachoonekana kuwa nafasi yake ya mwisho kutwaa Kombe la Dunia baada ya msimu mzuri akiwa na Bayern Munich.

Kane alifunga mabao 58 katika michezo 50 huku Bayern ikitwaa taji la Bundesliga na kukosa kwa karibu kufika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Kimataifa ameiongoza Uingereza kuwa moja ya timu zinazowania mataji mara kwa mara, lakini bado hajamaliza ukame wa miaka 60 wa taifa hilo kutoshinda taji kubwa.

Mara nyingi Kane amekuwa akisumbuliwa kimwili katika mashindano makubwa kutokana na uchovu wa msimu akiwa naklabu.

Hata hivyo, safari hii dakika zake za kucheza zimedhibitiwa na Bayern kwa miezi kadhaa walipoweka nguvu kubwa kwenye Ligi ya Mabingwa huku Bundesliga ikiwa tayari imeshinda.

Lamine Yamal (Hispania)

Lamine Yamal, winga wa Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania.
Lamine Yamal, winga wa Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania. © AP – Joan Monfort

Nyota aliyeibuka katika ushindi wa Hispania kwenye kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2024, matumaini ya Yamal kung’ara duniani yatategemea kupona kwake kutokana na jeraha la misuli ya nyuma ya paja.

Mchezaji huyo mwenye miaka 18 hajacheza tangu apate jeraha hilo akiwa na Barcelona Aprili 22 na huenda akakosa mechi mbili za kwanza za Hispania dhidi ya Cape Verde na Saudi Arabia.

Baada ya mwanzo wa msimu usioridhisha, Yamal alikuwa katika kiwango cha juu kabla ya kuumia, akifunga mabao 24 katika mashindano yote huku Barca ikitwaa taji la pili mfululizo la La Liga.

Hispania ina imani ya kuvuka hatua za mwanzo za mashindano kabla ya kumtumia nyota huyo ambaye wengi wanamchukulia kuwa mchezaji bora duniani katika hatua za mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *