Mkuu wa ujasusi wa Trump ajiuzulu kwa mashinikizo ya White House kuhusu vita haramu dhidi ya IranMkuu wa ujasusi wa Trump ajiuzulu kwa mashinikizo ya White House kuhusu vita haramu dhidi ya Iran

Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa (DNI) wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Tulsi Gabbard, amejiuzulu kutokana na shinikizo kubwa la Ikulu ya White House baada ya kupinga vikali vita haramu na vya uchokozi vya Marekani dhidi ya Iran.

Gabbard, ambaye aliongoza jumuiya kubwa ya ujasusi ya Marekani na kuratibu shughuli za ujasusi katika mashirika mengi ya ujasusi ya nchi hiyo, ametaja rasmi ugonjwa mbaya wa mumewe kama sababu ya kujiuzulu.

Katika barua ya kujiuzulu iliyochapishwa kwenye X Ijumaa, Tulsi Gabbard alitangaza kwamba Abraham Williams alikuwa amegunduliwa na aina mbaya na adimu ya saratani ya mifupa.

Hata hivyo, vyanzo vingi vinavyofahamu jambo hilo kwa undani vimethibitisha kwa Reuters kwamba chanzo halisi cha kuondoka kwake ni mashinikizo yanayoongezeka kutoka Ikulu ya Rais wa Marekani baada ya Gabbard kupinga vikali na mara kwa mara uamuzi usiofaa wa Marekani na Israel wa kuanzisha vita dhidi ya Iran bila “tishio lolote la karibu” kwa usalama wa Marekani.

Marekani na utawala wa Israel zilianzisha vita haramu vya uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Februari 28.

Mashambulizi hayo ya kijeshi yaliyokabiliwa na lawama nyingi za kimataifa, yamepandisha pakubwa bei za nishati na chakula duniani, na kusababisha maumivu makali ya kiuchumi kwa Wamarekani wa kawaida.

Kujiuzulu kwa Gabbard kunadhihirisha zaidi mgawanyiko mkubwa na wasiwasi unaoongezeka ndani ya utawala wa Trump kuhusu vita vya kipuuzi na vya gharama kubwa dhidi ya Iran.

Gabbard ni afisa wa nne mwanamke katika ngazi ya Baraza la Mawaziri kuondoka katika utawala wa Trump, kufuatia kujiuzulu aliyekuwa Waziri wa Kazi, Lori Chavez De Remer, Mwanasheria Mkuu Pam Bondi, na aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Kristi Noem.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *