
Iran imeishutumu siku ya Jumamosi, Mei 23, Marekani kwa kuhujumu mazungumzo ya kukomesha vita kwa “misimamo inayokinzana na madai ya mara kwa mara.” Mambo haya “yanavuruga mchakato wa mazungumzo yanaoongozwa chini ya usimamizi wa Pakistan,” amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi. Mabadiliko ya mipango ya Donald Trump, baada ya kusitisha kuhudhuria katika harusi ya mwanawe mkubwa, yanachochea uvumi kuhusu kuanza tena kwa uhasama.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amelalamika kuhusu “misimamo inayokinzana na madai ya mara kwa mara ya Marekani,” kulingana na mashirika ya habari ya Tasnim na FARS.
Mambo haya “yanavuruga mchakato wa mazungumzo unaoongozwa na Pakistan,” Araghchi amesema. “Licha ya kutoaminiana kwake sana na Marekani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeshiriki katika mchakato huu wa kidiplomasia kwa hisia ya uwajibikaji na uzito mkubwa, na inajitahidi kufikia matokeo yanayofaa na ya usawa,” ameongeza.
Siku iliyotangulia, Donald Trump alihakikisha kwamba Marekani hatimaye ingekamata uranium iliyorutubishwa ya Iran na kuiharibu. Kisha, katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa, alitangaza kwamba Iran “inatamani” kufikia makubaliano ya amani.
Ingawa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kilidai kwamba meli 35 zilivuka Mlango-Bahari wa Hormuz katika saa 24 zilizopita, afisa wa Falme za Kiarabu alikadiria kwa “50-50” uwezekano wa Marekani na Iran kufikia makubaliano ya kufungua eneo hili la kimkakati la baharini.
