Uganda imethibitisha visa vitatu vipya ya Ebola, na kufikisha idadi ya watu walioambukizwa kuwa watano tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha Ebola katika taifa hilo la Afrika Mashariki Mei 15.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na Wizara ya afya ya Uganda, wagonjwa wapya walioambukizwa ni dereva raia wa Uganda, mhudumu wa afya raia wa Uganda na mwanamke mmoja raia wa DRC.
Aidha Wizara ya afya ya Uganda imesema inaendelea kuimarisha juhudi za kupambana na kudhibiti msambao wa virusi hivyo, ikiwataka Waganda wote kuchukua tahadhari.
Hatua hii inajiri wakati huu Shirika la afya duninai WHO likiwa likionya kuhusu uwezekano wa virusi vipya vya Ebola kusambaa zaidi.
Alhamisi ya wiki, Uganda ilitanagaza kusitisha shughuli zote za usafiri wa umma kwenda nchini DRC kama njia moja ya kudhibiti msambao wa Ebola.
