
Angalau watu 24 wameuawa leo Jumapili katika shambulio la bomu kwenye treni iliyokuwa imewabeba wanajeshi katika jimbo lenye vurugu la kusini-magharibi mwa Balochistan, afisa mkuu amesema.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wanajeshi walikuwa miongoni mwa waathiriwa wa shambulio hilo, lililotokea katika mji mkuu wa mkoa, Quetta, na pia kuwajeruhi watu zaidi ya 50.
Treni hiyo, iliyokuwa imebeba wanajeshi na maafisa wa polisi waliokuwa wakielekea nyumbani kwa ajili ya likizo ya Eid, imeondoka Quetta Cantonment wakati mlipuko ulipotokea yapata saa 2:05 asubuhi kwa saa za Pakistan, vyanzo vya polisi vimesema kwa sharti la kutotajwa jina.
Mabehewa kadhaa yalipoteza njia na mawili yakashika moto kufuatia mlipuko huo, ambao pia uliharibu magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu na eneo la tukio. Wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa waliofariki na kujeruhiwa, vyanzo hivyo vimeongeza.
Watu hamsini na saba waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali ya kijeshi na 25 katika hospitali ya kiraia huko Quetta.
Kulingana na vyanzo kadhaa, uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa shambulio hilo lilifanywa kwa kutumia bomu lililotegwa ndani ya gari iliyokuwa na zaidi ya kilo 70 za vilipuzi.
