Wabunge kumchagua Spika mpya nchini UgandaWabunge kumchagua Spika mpya nchini Uganda

Nchini Uganda, wabunge leo Jumatatu, wanatarajiwa kumchagua Spika mpya, baada ya kuapishwa wiki moja iliyopita, kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Januari mwaka huu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi Jacob Oboth Oboth anatarajiwa kuchaguliwa kuwa Spika mpya, baada ya chama tawala NRM chini ya rais Yoweri Museveni, kuidhinisha jina lake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hii inakuja baada ya kujiondoa kwenye kinyanganyiro hicho aliyekuwa Spika Anita Among, ambaye amekabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi.

Wachambuzi wa siasa wanasema, jina la Oboth Oboth limepitishwa na chama cha NRM kufuatia ushawishi wa Mkuu wa Majeshi Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa kiume wa rais Museveni.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni baada ya kuapishwa kuongoza kwa muhula wa saba.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni baada ya kuapishwa kuongoza kwa muhula wa saba. REUTERS – Abubaker Lubowa

Kupitia  mtandao wake wa kijamii wa X kuwa, Kainerugaba alisema Waziri huyo wa ulinzi alikuwa mtu sahihi kuwa Spika katika bunge hilo jipya kitendo ambacho kinaonekana kushawishi hatua ya chama kulipitsha jina lake.

Kupigiwa kuwa kwa Oboth kunatarajiwa kuonekana kama kuidhinishwa tu na wabunge wa NRM ambao ndio wengi, baada ya rais Museveni kumuunga mkono kama Spika ajaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *