
Rais wa Marekani Donald Trump, amewaagiza wajumbe kutoka nchi yake, wasiwe na haraka ya kusaini mkataba wowote na Iran, licha ya hapo awali kudai kuwa mwafaka ulikuwa unakaribia kupatikana.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, rais Trump amesema mazungumzo mazuri yanaendelea lakini akasisitiza kuwa pande zote lazima, zichukue muda ili kupata mkataba sahihi.
Kauli ya hivi punde ya Trump, inakuja baada ya Jumamosi iliyopita, kudokeza kuwa, kwa kiasi kubwa mkataba huo ulikuwa umejadiliwa na kukubaliwa, akiashirikia kuwa wakati wowote, mwafaka unaweza kutangazwa.
Maafisa wa Iran kupitia msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje Esmail Baghaei nao wamesema pande hizo mbili zinakaribia au bado ziko mbali kupata mwafaka.
Ripoti zinasema, miongoni mwa masuala makubwa yanayojadiliwa ni pamoja na Iran kutaka Marekani, kuachia Akaunti zake za fedha, kuiondolea vikwazo, huku Washington ikitaka Tehran kuachana kabisa na mradi wake wa nyuklia.
