Rais wa China aunga mkono diplomasia ya amani kati ya Iran na MarekaniRais wa China aunga mkono diplomasia ya amani kati ya Iran na Marekani

Katika kikao chake na Waziri Mkuu na Mkuu wa Majeshi wa Pakistan, Rais wa China amesisitiza uungaji mkono wa Beijing kwa upatanishi wa Islamabad na diplomasia inayoendelea katika eneo la Magharibi mwa Asia kwa ajili ya amani, akitolea mfano ziara ya hivi karibuni ya Asim Munir, Mkuu wa Majeshi wa Pakistan jijini Tehran.

Shirika la habari la IRNA limevinukuu vyombo rasmi vya habari vya Pakistan na kuripoti kuwa, Shahbaz Sharif na ujumbe wake wa ngazi za juu Jumatatu walikutana na kuzungumza Rais Xi Jinping wa China huko Beijing.

Waziri Mkuu wa Pakistan ametilia mkazo nafasi muhimu ya China katika siasa za nje za Pakistan na kusisitiza kuwa, uwezo wa kiuchumi na kijeshi wa China unabeba ujumbe wa amani na usalama kwa dunia, kwa sababu Beijing inaunga mkono ulimwengu wa pande kadhaa kimataifa.

Ameongeza kuwa: “Pakistan inaimarisha uhusiano wake na China na inaamini kuwa uhusiano wa nchi mbili hauwezi kulinganishwa na chochote.”

Rais Xi Jinping wa China ameeleza kufurahishwa kwake na ziara ya Waziri Mkuu wa Pakistan na kuwepo kamanda wa jeshi la nchi hiyo mjini Beijing na kusema: “Tuna taarifa kuhusu vikao vya Asim Muniz mjini Tehran.”

Waziri Mkuu wa Pakistan Shahbaz Sharif jana Jumatatu alikutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake rasmi nchini China.

Kufuatia ziara hiyo, Pakistan na China zimetia saini mikataba ya ushirikiano yenye thamani ya dola bilioni 7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *