Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imeifuta rasmi na kuindoa mahakamani hati ya kesi ya madai iliyofunguli…Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imeifuta rasmi na kuindoa mahakamani hati ya kesi ya madai iliyofunguli…

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imeifuta rasmi na kuindoa mahakamani hati ya kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Kesi hiyo ilikuwa inahusu usawa kwenye mgawanyo wa mali za chama hicho kati ya Tanzania Bara na Zanzibar

Katika uamuzi wake wa leo Alhamisi uliotolewa mahakamani haoo kupitia kwa Jaji D. Ngunyale imeeleza kuwa wadai (waliofungua kesi) hawakuonesha -kifungu chochote kwenye hati y madai kinachoonesha kwamba uvunjifu huo (unaolalamikiwa na wadai) ulianza lini, jambo lililopelekea Mahakama kushindwa kujiridhisha kama ina mamlaka au la ya kuendelea kusikiliza kesi hiyo

Jaji Ngunyale amesema hati ya madai ilikuwa ina mapungufu makubwa, hivyo pingamizi lililowekwa na CHADEMA lina msingi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *