
Gazeti la Washington Post limeandika kuwa: Vita vya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza, Lebanon, Syria, Iran na Yemen vimeiweka Israel katika njia ya mmomonyoko wa kijeshi, kushindwa kimkakati na kutengwa kimataifa.
Washington Post linasisitiza katika ripoti yake kwamba: Baada ya Oktoba 7, 2023 (Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa), Netanyahu alijitenga na sera ya awali; na kupitia sera ya vita mfululizo, amejaribu kubuni upya ramani ya Asia Magharibi; lakini mbinu hii haikufanikiwa kufikia malengo yake yaliyotangazwa, lakini pia imepunguza sana uungwaji mkono wa kimataifa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Ripoti hiyo inaongeza kuwa malengo ya Netanyahu nchini Iran, ikiwa ni pamoja na kuharibu mpango wa nyuklia wa amani na kuondoa madarakani utawala wa nchi hiyo, yameshindwa, na Tehran imejibu kwa kudhibiti Mlango-Bahari wa Hormuz. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utawala wa Kizayuni sasa unategemea sana na kwa njia hatari usaidizi wa kijeshi wa Marekani, huku uungwaji mkono wake ndani ya Marekani ukishuka hadi kiwango kisicho na kifani.
Gazeti la Washington Post limehitimisha kwamba jaribio la Netanyahu la kupata usalama kamili kupitia nguvu za kijeshi pekee limekuwa na matokeo kinyume na linaharibu usalama na nguvu za utawala wa Israel kwa muda mrefu.
