Wawili Serengeti Boys waongezwa Taifa StarsWawili Serengeti Boys waongezwa Taifa Stars

Dar es Salaam. Benchi la ufundi la Taifa Stars, limewaongeza kikosini wachezaji wawili wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ baada ya kukoshwa na viwango wanavyoonyesha katika Fainali za Mataifabya Afrika (AFCON U17) zinazoendelea Morocco.

Wachezaji hao ni mshambuliaji Luqman Mbalasalu na beki Kassim Juma.

Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema kuwa wawili hao watakuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars katika mechi mbili za kirafiki dhidi ya Uganda na Rwanda mwezi ujao.

Mechi hizo ambazo zipo katika kalenda ya FIFA, ya kwanza itakuwa Juni 5 dhidi ya Uganda na Juni 9 dhidi ya Rwanda.

Katika fainali hizo, Luqman amechangia mabao mawili ambapo amefunga baomoja na kupiga pasi moja ya mwisho.

Kwa upande wa Kassim Juma amekuwa mchezaji tegemeo katika safu ya ulinzi ya Serengeti Boys ambayo haijaruhusu bao katika mechi tatu kati ya tano ilizocheza za mashindano hayo.

Kassim Juma pia ndio nahodha wa kikosi cha Serengeti Boys ambacho kimetinga hatua ya fainali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *