
Kamanda wa cheo cha juu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) anasema Rais wa Marekani, Donald Trump, hana chaguo zuri kuhusu Iran na anapaswa kuchagua kati ya njia “mbaya” au “mbaya zaidi”.
“Trump, ambaye kushindwa kwake katika vita kumedhihirika kwa watu wote, sasa anakabiliwa na njia mbili: Njia mbaya au mbaya zaidi,” amesema Naibu wa Masuala ya Siasa wa IRGC, Brigedia Jenerali Yadollah Javani.
Javani ameharakisha kuongeza kwamba rais wa Marekani lazima achague kati ya kutambua masharti na haki za taifa la Iran au kuendelea na vita vya uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Amesisitiza kwamba adui amefanya kosa la kimkakati katika hesabu zake za kuanzisha vita vya uchokozi dhidi ya taifa la Iran.
“Iran imeshinda vita hivi, na Marekani inabakia katika mzunguko wa kushindwa na kushuka,” Javani amesema.
Kamanda huyo wa ngazi za juu wa IRGC ameongeza kwamba Washington na utawala wa Tel Aviv walifanya mashambulizi makubwa na yasiyo na sababu dhidi ya Iran wakidhani watapata ushindi katika muda wa siku chache, huku malengo yao ya kimkakati yakijumuisha kuangamiza uwezo wa nyuklia wa nchi, kuharibu uwezo wake wa makombora, na hatimaye kupindua utawala wa Kiislamu.
Ameashiria mabadiliko yanayoshuhudiwa katika milinganyo ya kikanda kwa maslahi ya Iran, akisema kwamba Jamhuri ya Kiislamu sasa inadhibiti kikamilifu Mlango-Bahari wa kimkakati wa Hormuz, na imerejesha hadhi na haki halali ya taifa la Iran baada ya miaka 500.
“Iran sasa iko katika nafasi ya ushindi na ubora. Jamhuri ya Kiislamu imetangaza masharti yake ya kuvunja mkwamo uliopo, na sasa ni zamu ya Marekani kufanya uamuzi kuhusu jambo hilo,” amesema Javani.
“Kuna makubaliano kati ya vikosi vya jeshi, wanadiplomasia na wananchi kutoka matabaka yote ya jamii kwamba haki za taifa la Iran lazima zitimizwe, iwe ni kupitia mazungumzo na makubaliano, au njia nyingine,” amesisitiza Javani.
Kamanda huyo wa ngazi za juu wa IRGC hatimaye ameonya dhidi ya makosa yoyote zaidi ya adui, akisisitiza kwamba vikosi vya jeshi la Irani vimejiandaa kikamilifu, na majibu yao yatakuwa na makali zaidi, yenye uamuzi zaidi, na yasiyofikirika zaidi iwapo adui atafanya kosa jingine.
Love how you make learning enjoyable and engaging for absolutely everyone here