Dar es Salaam. Bei ya mafuta ya Petroli imeshuka wa Sh29 kwa Dar es Salaam na sasa itakuwa Sh4,086  kutoka Sh4,115 na dizeli ikipanda kwa Sh85 baada ya kuwekewa ruzuku ya Sh534 kwa lita.

Baada ya ruzuku hiyo, dizeli kwa mafuta yanayopita bandari ya Dar es Salaam itauzwa Sh4,333 kutoka Sh4,248 iliyokuwapo Mei 2026.

Bei hizo zimetolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ambazo zitaanza kutumika leo Jumatano, Juni 3, 2026.

Taarifa ya Ewura iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Gerald Maganga imeeleza mabadiliko ya bei za mafuta nchini kwa Juni 2026 yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na vita inayoendelea eneo la Mashariki ya Kati, iliyoanza tarehe 28 Februari 2026, ikihusisha nchi za Marekani, Israeli na Irani.

Maganga amesema kwa kuwa Tanzania inaagiza sehemu kubwa ya mafuta yake kutoka nchi za Mashariki ya Kati, athari za mabadiliko hayo ya kimataifa zimejitokeza moja kwa moja katika soko la ndani.

“Miongoni mwa hatua hizo ni utoaji wa ruzuku ya takriban Sh534.91 kwa kila lita moja ya mafuta ya dizeli. Mafuta ya dizeli ni muhimu katika shughuli za kiuchumi na kijamii zikiwemo uzalishaji viwandani, usafirishaji wa bidhaa na huduma za usafiri wa umma,” amesema.

Kwa upande wa mafuta ya taa yanayopita Bandari ya Dar es Salaam yatanunuliwa kwa Sh4,685 kutoka Sh4,677 iliyokuwa ikitumika Mei mwaka huu ikiwa ni ongezeko la Sh8.

Kwa upande wa watumiaji wa petroli inayopitia katika Bandari ya Tanga, lita moja itauzwa kwa Sh4,157 kutoka Sh4,176 ikiwa ni ongezeko la Sh19 kwa kila lita.

Wanaotumia mafuta ya dizeli yanayopita katika bandari hiyo sasa watanunua lita moja kwa Sh44,04 kutoka Sh4,309 ikiwa ni ongezekoo la Sh95 kwa lita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *