
Mkutano huu unaweza kuzua hisia jijini Dakar. Siku ya Jumanne, Juni 2, Emmanuel Macron amempokea rais wa zamani wa Senegal Macky Sall katika Ikulu ya Élysée. Mkutano huo, uliorushwa na Sall kwenye mitandao ya kijamii, ulihusu kugombea kwake kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkutano huo haukuwa kwenye ajenda rasmi ya rais wa Ufaransa. Hata hivyo, Macky Sall mwenyewe aliupa mkutano huo uzito fulani kwa kurusha picha kwene motandao ya kijamii siku ya Jumatano, Juni 3, zikimuonyesha akiwa pamoja na rais Emmanuel Macron. Katika picha hizo, zilizopigwa siku moja kabla, wawili hao wanaonekana wakishikana mikono kwenye ngazi kubwa ya Ikulu ya Élysée.
“Ninamshukuru kwa dhati rais Emmanuel Macron kwa makaribisho yake mazuri na mazungumzo yetu mazuri,” aliandikarais huyo wa zamani wa Senegal katika ujumbe uliochapishwa kwa Kifaransa na Kiingereza. “Tunashiriki maono ya Umoja wa Mataifa wenye matamanio, mageuzi na ufufuo ili kuimarisha ufanisi wake, uwakilishi na uwezo wa kukidhi matarajio ya watu na mataifa,” aliongeza.
Baada ya kuhojiwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi Aprili kuhusu kugombea kwake kwenye nafasi ya Katibu Mkuu, Macky Sall alipendekeza mageuzi ya Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia kanuni tatu: “kupanga upya, kurahisisha, na kuboresha.”
Ikulu ya Élysée haikutoa haikuzungumza chochote kuhusu mkutano huu, wala kuhusu uwezekano wowote wa Ufaransa wa kuunga mkono rais wa zamani wa Senegal kuwania kwenye nafasi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, mkutano huu unathibitisha uhusiano mzuri kati ya Emmanuel Macron na Macky Sall.
Kugombea bila uungwaji mkono rasmi kutoka Senegal
Rais wa zamani wa Senegal anaendesha kampeni yake ya kimataifa bila uungwaji mkono rasmi kutoka nchi yake. Mapema mwezi Mei, Rais Bassirou Diomaye Faye alieleza kwamba Dakar ilichagua “msimamo usioegemea upande wowote.” “Hatujashirikishwa tangu mwanzo, hata na mhuska mwenyewe, Macky Sall,” rais wa Senegal alitangaza.
Nchini Senegal, mkutano huu katika Ikulu ya Élysée ulizua hisia mbalimbali na wafuasi wa rais wa zamani. Néné Tall, mwanachama wa chama cha Alliance for the Republic, alishiriki picha ya mkutano huo, akiandika: “Wakati huo huo, watu mashuhuri wanajadili mustakabali wa dunia.”
Taarifa hiyo pia iligonga vichwa vya habari katika vyombo kadhaa vya habari vya mtandaoni vya Senegal. Tovuti ya Dakar Actu, haswa, inabaini kwamba “uungwaji mkono, au angalau nia njema, ya Paris ina faida kubwa katika kinyang’anyiro cha kumrithi Antonio Guterres.” Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa atachukua madaraka Januari 1, 2027. Atachaguliwa wiki chache mapema.