Mapigano yameanza usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi mjini Mogadishu, ambapo moshi mwingi unaonekana katika mji mkuu wa nchi hiyo, kulingana na waandishi wa habari wa shirika la habri la AFP. Polisi ya Somalia imetangaza operesheni kubwa dhidi ya “wanamgambo.”

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Operesheni kubwa ya usalama inayofanywa na vikosi vya usalama vya mji mkuu inakaribia kukamilika. Operesheni hii inalenga kuwaangamiza wanamgambo wenye silaha kali ambao wameanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya baadhi ya vitongoji vya mji mkuu,” polisi imeandika katika taarifa.

Siku ya Jumatano, vikosi vya jeshi la serikali na wanamgambo wenye silaha walirushiana risasi katika mji wa Mogadishu. Waziri Mkuu wa zamani wa Somalia Hassan Ali Khaire amedai kuwa mwathiriwa wa shambulio la vikosi vya serikali. Msemaji wa polisi ya Somalia Abdifatah Adan, kwa upande wake, amesema kwamba maafisa wa polisi “walishambuliwa na wanamgambo.”

Uchaguzi ulipangwa kufanyika Juni, lakini sasa inaonekana kuwa vigumu uchaguzi huo kufanyika

Somalia imerudi katika mgogoro wa wazi, wiki mbili baada ya rais Hassan Sheikh Mohamud (HSM) kuruhusiwa kusalia madarakani licha ya muhula wake kumalizika. Mnamo mwezi Machi, serikali ilipitisha mageuzi ya kikatiba yaliyoanzisha uchaguzi wa moja kwa moja kwa wabunge na kuongeza muhula wa rais na wa wabunge kutoka miaka minne hadi mitano.

Kambi ya rais inabaini kwamba muhula wa rais Hassan Sheikh Mohamud umeongezwa kwa mwaka mmoja. Lakini upinzani unabaini kwamba mageuzi haya ni njia ya yeye kushikilia madaraka na umeitisha maandamano leo Alhamisi. Uchaguzi ulipangwa kufanyika Juni, lakini sasa inaonekana kuwa ni vigumu uchaguzi huo kufanyika. Nchi hiyo imekuwa ikikabiliana kwa karibu miaka 20 na uasi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al Shabab, lenye uhusiano na al-Qaeda, ambalo linadhibiti maeneo makubwa nchini Somalia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *