Nigeria inapanga kuwarejesha nyumbani raia wake zaidi ya Elfu 1 kutoka Afrika Kusini ,wakati huu machafuko na mashambulizi yanayohusishwa na chuki dhidi ya wageni na wenyeji ,yakiendelea.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inajiri baada ya Ghana kuchukua mpango kama huu wa kuwaresha nyumbani raia Wake karibu 800.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje, Kimiebi Ebienfa,amesema tayari ukaguzi wa khiari wa raia wanaotaka kurudi nyumbani umeanza kuznia siku ya Alhamisi.

Ubalozi wa Nigeria jijini Pretoria, umesema ,unashauriana na mamlaka nchini Afrika Kusini ili raia wa Nigeria ambao wanakabiliwa na makosa ya kukiuka sheria za uhamiaji wanaweza kusamehewa na kuruhusiwa kuondoka badala ya kukamatwa.

Serikali ya Afrika Kusini imeendelea kusema inaimarisha msako wa wahamiaji haramu ili imewataka wananchi kutochukua sheria mkononi.

Kuna wahamiaji zaidi ya milioni tatu wanaoishi Afrika kusini ,asilimia 63 wakiwa ni wananchi kutoka nchi wanachama wa muungano wa kimaendeleo wa nchi za Afrika Kusini ,SADC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *