
Israel na Iran zimekabiliana siku ya Jumatatu kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa kipindi cha usitishaji wa mapigano mashariki ya kati miezi miwili iliopita.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Makabiliano kati ya pande hizo mbili yameripotiwa licha ya wito wa Rais Trump kuzitaka kutoshambuliana.
Iran iliishambulia Israeli katika kile ilisema ni kujibu hatua ya Israeli kuendelea kutekeleza mashambulio kusini mwa Beirut, eneo ambalo ni ngome ya wapiganaji wa Hezbollah ambao ni washirika wa Iran.
Israeli kwa upande wake ilichukua hatua ya kulipiza kisasi ikitekeleza mashambulio makubwa katika Miji mbalimbali nchini Iran ikiwemo jijiji Tehran.
Mashambulio hayo yamejiri kufuatia wiki kadhaa za mazungumzo ya kujaribu kupata mkataba wa kudumu kumaliza vita mashariki ya kati ambavyo vilianza Februari 28 baada ya Marekani na Israeli kuishambulia Iran.
Licha ya makabiliano, hadi tukichapisha taarifa hii, hakuna upande uliokuwa umeripoti vifo vyovyote vilivyotokana na mashambulio hayo mapya.
Israeli imesema imeshambulia na kuharibu mifumo ya ulinzi wa angani wa Iran katika Miji mbalimbali.
Aidha imesema imeshambulia kiwanda cha mafuta cha Iran, wapiganaji wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nao wakishambulia Israeli kwa makombora.