Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amezuru Uganda na kukutana na maafisa wakuu wa afya nchini humo huku taifa hilo likiendelea kukabiliana na mlipuko wa Ebola ambao tayari umesababisha vifo vya watu wawili baada ya kuenea kutoka nchi jiran ya DRC.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo inajiri siku chache baada ya Tedros kutembelea DRC, ambako mlipuko wa sasa wa Ebola umeambukiza watu 515 na kusababisha vifo 91.

Akizungumza mjini Kampala, Tedros amesema WHO, kwa ushirikiano na kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa CDC wameimarisha msaada kwa Uganda ili kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Ebola huenezwa kupitia mgusano wa karibu na mtu aliyeambukizwa au majimaji ya mwili wake. Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, ugonjwa huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 15,000 barani Afrika.

Wakati huo huo, WHO Ijumaa iliyopita ilizindua mpango wa dharura wa dola milioni 518 za Marekani kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko huo katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *