
Mgogoro wa mafuta duniani uliochangiwa na vita kwenye eneo la mashariki ya kati, unaonesha namna dunia inapaswa kuachana na utegemezi wa mafuta ya visukuku na kuelekea kutumia nishati safi, hii ni kwa mujibu wa wataalamu wa mazingira na hali ya hewa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wito wa wataalamu hawa umekuja ikiwa imesalia miezi michache kabla ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa wa COP31 nchini Uturuki.
Wataalamu wanaokutana mjini Berlin, kuelekea kongamano la COP31, wameoanisha vita kati ya Iran na Marekani ambayo imeathiri ugavi wa mafuta duniani na haja ya mataifa kubadilika na kuanza kutumia nishati jadidifu.
Mkuu wa masuala ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa Simon Stiell, amesema vita inayoendelea imeleta tabú kwa rai ana kusababisha bei ya nishati ya mafuta kupanda maradufu na kwamba kuendelea kutegemea mafuta ya visukuku kunamaanisha kuendelea kusababisha mfumuko wa bei na mgogoro wa kiuchumi.
Nchi ya Uturuki ambayo itakuwa mwenyeji wa mkutano wa COP31 huko Antalya mwezi November na Australia ambayo yenyewe itaongoza majadiliano, kwa kauli moja zimeonya kuhusu madhara ya vita inayoendelea na hatari ambayo dunia itashuhudia kutokana na Athari za mabadiliko ya tabianchi.