Bondia Hassan Mwakinyo maarufu Champez usiku wa kuamkia leo amepigwa KO na mpindani wake Michel Soro wa Ivory Coast kwenye pambano la kuwania mkanda wa (IBO) wa dunia udhani wa kati (Middleweight).

Mwakinyo alipanda ulingoni katika pambano la raundi 12 akisaka rekodi mpya kwenye ngumi za kulipwa, lakini alishindwa kuhimili uzoefu wa Soro ambaye alimdhibiti kwa sehemu kubwa ya pambano kabla ya mwamuzi kulisitisha katika raundi ya tisa na kumpa ushindi kwa TKO ambapo kabla ya pambano hilo rekodi za mabandia hao zilikuwa zinaonesha kuwa

Soro raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 38, amepanda ulingoni mara (44), akishinda mapambano 38 (akipata KO 27), akipigwa mara (4) na akitoa sare mara (2).

Wakati Mwakinyo ana rekodi ya kupigana mapambano mara (28) akishinda mapambano (25) kati ya hayo (18) ameshinda kwa (KO) na akipigwa mapambano matatu (3)

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *