Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu umewapandisha kizimbani Mhitimu mmoja na wanafunzi 17 wa vyuo vikuu na vyuo vya kati mbalimbali jijini Dar es Salaam wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kughushi nyaraka na kujipatia mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kwa njia ya udanganyifu.
Washitakiwa hao walisomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali, Titus Aaron akisaidizana na Cathbert Mbilingi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya.
Wakili Titus alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na jumla ya makosa 47 yakiwemo ya kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za uongo na kujipatia mikopo kwa njia ya udanganyifu kinyume na vifungu mbalimbali vya Kanuni ya Adhabu.
Kesi iliahirishwa hadi Julai 9,mwaka huu kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.
(Feed generated with FetchRSS)