#HABARI: Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema maboresho makubwa yamefanyika katika Kiwanja cha Ndege cha Arusha, na kinatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.

Dkt. Samia ameeleza kuwa baada ya kukamilika, kiwanja hicho kitaanza kutumika rasmi Januari 2026 kwa kufanya kazi saa 24, hatua hiyo itarahisisha safari za watalii, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Dkt. Samia ametaja maboresho mengine katika Kiwanja cha Ndege cha Ziwa Manyara, Karatu, ambako zaidi ya Shilingi milioni 88.5 zimetumika kujenga barabara ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 1,500 kwa kiwango cha lami pamoja na jengo la abiria.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetan

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *