Nyota wa zamani wa soka wa Misri na mchambuzi wa masuala ya michezo, Mohamed Aboutrika, ameibua wimbi kubwa la majibizano na mijadala kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kukosoa sera za undumakuwili katika kuandaa mashindano makubwa ya michezo, na jitihada za baadhi ya nchi za kutumia michezo kama wenzo wa kutakasa na kusafisha sura zao chafu za kisiasa.

Katika video iliyovutia watazamaji wengi, Mohamed Aboutrika amesema kwamba mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar la 2022 yanasalia kuwa mashindano yaliyopangwa vyema zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.

Nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Misri ameshambulia vikali matoleo ya huko nyuma ya Kombe la Dunia, akisisitiza kwamba yeyote anayetaka kuosha sura yake chafu ya kisiasa anaamua kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia, akimaanisha nchi kubwa zinazoshiriki katika vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, kupigana vita na nchi zingine, na baadhi yao hata zilikwenda mbali na na kumteka nyara rais nchi nyingine, kisha zinajitokeza sasa kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia kwa kisingizio cha kueneza demokrasia!

Nyota huyo wa zamani wa Mafarao ametabiri kwamba toleo la sasa la Kombe la Dunia litakumbwa na matatizo makubwa ya kiufundi na ya kimfumo, ikieleza kwamba baadhi ya migogoro hiyo ilianza kuonekana hata kabla ya sherehe ya ufunguzi.

Mohamed Aboutrika ameongeza kuwa: “Tutashuhudia Kombe la Dunia lililofeli zaidi, kwa sababu matatizo yalianza kuonekana kwa kuzuiwa waamuzi, matatizo ya viwanja, matatizo ya hali ya hewa, na matatizo ya upangaji.”

Kauli hii imeibua wimbi la mijadala mikali miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhusu suala la kusiasisha mpira wa miguu.

Katika muktadha huu, mtangazaji wa Algeria, Ania ametangaza uungaji mkono wake kamili kwa matamshi ya Aboutrika, akiandika kwenye Twitter kwamba, walimwengu hawatasahau uhalifu uliotokea katika Ukanda wa Gaza, na amepinga wito wa kutenganisha siasa na michezo linapokuja suala la watu wa Gaza tu.

Mtumiaji wa Twitter, Oman, Brir Al Lawati, ameeleza kwamba nchi za Magharibi ndizo zilizoanza kuingiza siasa katika soka na kuitumia kama wenzo, akitoa mfano wa kususiwa Urusi katika Kombe la Dunia na michuano ya Ulaya, na kampeni kubwa ya mashinikizo iliyoanzishwa dhidi ya Qatar katika mashindano ya Kombe la Dunia la 2022 kwa kisingizio cha kutetea ushoga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *