Karibu mashirika 100 ya mazingira yametoa wito kwa wenyeji wenza wa mkutano wa hali ya hewa wa COP31 nchi za Uturuki na Australia “kuongoza kwa mfano” kwa kushughulikia utegemezi wao kwenye mafuta ya visukuku.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mataifa ya Uturuki na Australia kwa sehemu kubwa yamekuwa yakitegemea matumizi ya mafuta ya visukuku lakini yameahidi kugeukia matumizi ya nishati safii.

Katika barua kutoka kwa watetezi wa mazingira iliyotumwa kwa nchi hizo mbili, wanazitaka kuzungumzia changamoto kubwa inayoikabili mazingira ikiwa ni matumzi ya makaa, Petroli, diseli na gesi.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika wakati huu ambapo vita vya mashariki ya kati vikisababisha kupanda kwa bei ya nishati.

Uturuki itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mazingira mwezi Novemba wakati Australia kwa upande wake ikitarajiwa kuongoza majadiliano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *