
Mkuu wa Idara ya ujasusi wa Ethiopia na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa nchi hiyo wamesema kwamba shambulio hilo linaweza kutokea hivi karibuni. Dai hili lilikanushwa na kutajwa kuwa ni “uwongo mtupu” na kiongozi wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF), ambacho pia kinatawala eneo hilo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Miaka mitatu na nusu baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya Pretoria, tishio la vita vipya huko Tigray linaikabili Ethiopia. Katika tahariri iliyochapishwa siku ya Alhamisi, Juni 11, kwenye Al Jazeera, mkuu wa idara ya ujasusi wa Ethiopia, Redwan Hussein, na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Ethiopia, kiongozi wa zamani wa waasi wa Tigray Getachew Reda, wanashutumu vikosi vya Tigray kwa kupanga mashambulizi katika siku zijazo.
Shambulio hilo linasemekana hata kuwa karibu, kulingana na maafisa hawa wawili wakuu wa serikali ya shirikisho, ambao pia walishutumu muungano ulioundwa kati ya serikali ya Eritrea, vikosi vya Tigray, na vikosi vya waasi kutoka eneo jirani la Amhara. Waliuelezea muungano huu kama “uliounganishwa wakati wa mikutano ya hadhara nchini Ethiopia na Sudan,” kwa lengo la kudhoofisha makubaliano yaliyosainiwa mwaka wa 2022 nchini Afrika Kusini ambayo yalimaliza mgogoro wa miaka miwili kati ya pande hizo mbili.
Watu 600,000 waliangamia katika vita vya Ethiopia
Kwa upande wake, Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF), mamlaka ya upinzani katika eneo la Tigray, siku ya Ijumaa, Juni 12, kilijibu kauli hizi, kikizitangaza kuwa “si za kweli kabisa”. Kwa upande mwingine, Cjhama hicho kiliishutumu serikali ya shirikisho kwa kutafuta kisingizio cha kuanzisha vita vipya.
Katika juhudi za kutuliza mvutano uliokuwa ukiongezeka, Olusegun Obasanjo, rais wa zamani wa Nigeria aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika kama mpatanishi katika mgogoro huo, alisafiri hadi Tigray siku ya Alhamisi, Juni 11. Huko, alikutana na Debretsion Gebremichael, ambaye anaongoza eneo hilo na TPLF, na kufanya mazungumzo ili kuzuia kuanza tena kwa mgogoro huo.
Vita kati ya jeshi la shirikisho la Ethiopia na vikosi vya TPLF, vilivyotokea kati ya mwezi Novemba 2020 na mwezi Novemba 2022, inakadiriwa kuwa vilisababisha vifo vya watu wapatao 600,000.