Canada, mwenyeji mwenza wa Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2026 na Marekani na Mexico, imekataa kumpa visa mchezaji wa Ghana Thomas Partey, anayetuhumiwa kwa ubakaji nchini Uingereza ambapo atafika mbele y mahakaam mnamo mwaka wa 2027. Hili lilitangazwa siku ya Ijumaa, Juni 12, na FIFA, ikithibitisha ripoti za awali kwa vyombo vya habari.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Ghana itakuwa bila mmoja wa wachezaji wake muhimu kwa mechi yake ya ufunguzi katika Kombe la Dunia la 2026. Kufuatia ripoti kwenye vyombo vya habari, shirika la Soka duniani, FIFA, lenyewe lilitoa taarifa siku ya Ijumaa, Juni 12, siku moja baada ya michuano kuanza nchini Mexico: Canada inakataa kumpa Thomas Partey visa.

Ikiwa katika Kundi L, Black Stars imepangwa kucheza mechi yao ya kwanza ya Kombe hili la Dunia mnamo Juni 17 huko Toronto, Canada. Kisha watakabiliana na Uingereza mnamo Juni 23 huko Boston, Marekani, wakifuatiwa na Croatia huko Philadelphia, pia nchini Marekani. Kwa hivyo Thomas Partey hatakuwepo kwa mechi ya kwanza kwenye ardhi ya Canada. Kulingana na chanzo kilicho karibu na suala hilo kilichowasiliana na shirika la habari la AFP, ataweza kucheza katika mechi zingine mbili nchini Marekani.

“FIFA inaweza kuthibitisha kwamba Thomas Partey hataweza kusafiri kutoka Boston, ambapo timu ya taifa ya Ghana iko, kwenda Canada kwa mechi ya kwanza dhidi ya Panama siku ya Jumatano, Juni 17, kwani ombi lake la visa lilikataliwa na serikali ya Canada,” shirika hilo lilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari, likibainisha kwamba “halihusiki katika taratibu za uhamiaji za nchi mwenyeji” za Kombe la Dunia.

Kiungo huyo wa kati, ambaye amekuwa akichezea Villarreal nchini Uhispania kwa mwaka mmoja, amezuiliwa kuingia Canada kutokana na mashtaka ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia yaliyoletwa dhidi yake nchini Uingereza. Thomas Partey anatuhumiwa na wanawake wanne kwa matukio ambayo inadaiwa yalitokea kati ya mwaka 2021 na 2022, alipokuwa akichezea klabu ya Uingereza ya Arsenal. Amekana mashtaka saba ya ubakaji na shtaka moja la unyanyasaji wa kingono. Atafika mbele ya mahakaam mwaka wa 2027.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *