Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela, amewataka wasomi wa Mkoa wa Mbeya kuwa mabalozi wa kueleza mafanikio ya maendeleo yaliyofikiwa nchini.

Mwaselela ameyasema hayo, alipozungumza na wasomi wa Mkoa wa Mbeya.

Amesema wasomi wanapaswa kutumia taaluma na ushawishi wao katika jamii kufikisha taarifa sahihi kuhusu miradi ya maendeleo na mafanikio ya Serikali.

Ameeleza ni muhimu kwa wananchi kupata taarifa zinazojenga uelewa sahihi wa mwelekeo wa nchi badala ya kuongozwa na upotoshaji unaoweza kuvuruga mshikamano wa kitaifa.

Katika mkutano huo, amewahimiza wasomi walihimizwa kuwa walimu wa mazuri kwa jamii zao na kushiriki kulinda amani, utulivu na umoja wa Watanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *