
Waziri Mkuu wa Pakistan ametangaza Jumapili jioni, Juni 14, 2026, kwamba Marekani na Iran zimefikia makubaliano ya amani. Sherehe rasmi ya utiaji saini itafanyika siku ya Ijumaa, Juni 19, nchini Uswisi, kulingana na Pakistan, ambayo ni mpatanishi katika mzoo kati ya nchi hiei mbili. Kufuatia tangazo hili, Donald Trump ametangaza kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz na kuondolewa kwa kizuizi cha majini cha Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Pakistan kupitia Waziri wake Mkuu, imetangaza kwamba makubaliano yamefikiwa kati ya Marekani na Iran. “Kufuatia mazungumzo makali, tunafurahi kutangaza kwamba makubaliano ya amani kati ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamefikiwa. Pande zote mbili zimetangaza usitishaji mara moja na wa kudumu kwa shughuli za kijeshi katika pande zote, ikiwa ni pamoja na Lebanon.” “
Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump amebainisha siku ya Jumapili kwamba makubaliano ya kukomesha mgogoro katika Mashariki ya Kati yamekamilishwa na Iran na kutangaza kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz pamoja na kuondolewa mara moja kwa kizuizi cha jeshi la majini la Marekani.
“Makubaliano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa yamekamilika. Hongera kwa nyote! Ninaidhinisha bila masharti kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz na, wakati huo huo, kuondolewa mara moja kwa kizuizi cha jeshi la majini la Marekani. Meli za dunia nzima, washeni meli zenu. Na mafuta yatiririke kwa wingi!” amesema.