Marekani na Iran zimekubaliana kusitisha mapigano mara moja ambapo yatakuwa ni yakudumu, hatua inayotajwa kuwa mwisho wa zaidi ya miezi mitatu ya vita katika eneo la mashariki ya kati.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano haya ambayo yaliratibiwa na Pakistan yamethibitishwa na Washington pamoja na Tehran, ambapo yanatarajiwa kutiwa saini rasmi nchini Uswisi Ijumaa ya wiki hii.

Aidha Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kufunguliwa tena kwa Mlango bahari wa Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani, huku Iran kwa upande wake ikisema makubaliano hayo yanamaliza mara moja uhasama kati ya pande hizo.

Usitishaji huo wa mapigano pia unahusisha Lebanon, ambako mashambulio ya wikendi ya Israel yalitishia kuvuruga mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea.

Nchi za Ulaya, ikiwemo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italia zimekaribisha makubaliano hayo na kuonesha kuwa tayari kuondoa baadhi ya vikwazo dhidi ya Iran.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Iran, Marekani pia inatarajiwa kuachilia sehemu ya mali za Iran zilizokuwa zimezuiwa kwa miaka kadhaa, hatua inayotazamwa kama ishara ya kujenga imani kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya kina kuhusu mustakabali wa uhusiano wa nchi hizo mbili.

Tangazo la kupatikana kwa makubaliano limepokelewa kwa matumaini na jumuiya ya kimataifa, wakati huu pia bei ya mafuta kwenye soko la dunia ikishuka kwa zaidi ya asilimia nne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *