
Zaidi ya raia 1,000 wameuawa nchini Sudan mwaka huu kupitia ndege sizo na rubani, kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkurugezi mkuu anayeshughulikia haki za binadamu wa umoja wa mataifa, Volker Türk, amesema mashambulizi hayo yaliyorekodiwa kati ya Januari na Mei yanaonyesha kuwa vita nchini humo vimeongezeka na kwamba kutisha zaidi.
Onyo hilo linatolewa wakati watu wasiopungua 23 wakiripotiwa kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani yaliyolenga mji muhimu wa El Obeid.
Muungano mawakili wa huduma za dharura nchini Sudan limesema watu wanne waliuawa na 12 kujeruhiwa katika shambulizi lililolenga msafara mmoja wa mazishi, huku mashambulizi mengine yakisababisha vifo zaidi katika maeneo mbalimbali ya mji huo.
Mashirika ya msalaba mwekundu yamethibitisha kuwa mmoja wa wahudumu wake, Ahmed Yaqoub Othman, ni miongoni mwa waliouawa wakati akiwahudumia majeruhi wa mashambulizi hayo.